Mchezaji wa Tottenham Spurs Eric Dier amemshukuru Antonio Conte na wachezaji wenzake kwa kumsaidia kurejeshwa kwenye kikosi cha England ambacho anatumaini ni “hatua ya kuanzia tu”.

 

Dier Amshukuru Conte

Beki huyo wa Spurs Dier ameitwa na Gareth Southgate kwaajili ya mechi zijazo za ligi ya Mataifa dhidi ya Italia na Ujerumani. Mechi za hivi karibuni kati ya mechi zake 45 zilikuja Novemba 2020, lakini kuimarika kwa kiwango cha klabu kunamfanya Dier kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.

Uchezaji bora wa beki huyo ulikwenda sambamba na uteuzi wa Conte Novemba mwaka jana, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ana imani kwamba anaweza kuendeleza uwezo wake kuwa wa juu.

 

Dier Amshukuru Conte

Alisema anatazama mbele kwa sasa na anadhani kwamba anaweza kufanya mengi mazuri, pia alisema kuwa alichokuwa akifikiria ni kufanya vizuri pale Spurs na kila kitu kinachotokea ni matokeo yake.

“Ninashukuru kwa jinsi wachezaji wenzangu, wakufunzi na kila mtu Spurs ameniunga mkono, kunisukuma na kujaribu kunisaidia kurejea kwenye timu ya Taifa”.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa