Winga wa kimataifa wa England na Manchester City Raheem Sterling amepewa ofa ya mkataba wa udhamini kutoka kampuni ya vifaa vya michezo PUMA yenye thamani ya Pauni Milioni 100 (Bilioni 287 Tsh)
Hata hivyo kwa mujibu wa magazeti ya uingeleza, mazungumzo kati ya Sterling na Nike bado yanendelea na kunatazamiwa Nike wanaweza kuongeza mkataba na sterling unaotarajiwa kudumu mpaka mwaka 2023.

Vita ya Fedha ya kampuni hizo mbili zinaweza kumuweka sehemu nzuri kifedha mwanasoka huyo wa uingeleza kwa maana makampuni yote mawili yameweka dau linalofanana na hakika Kampuni itakayo ongeza dau ndio ita nasa Sahihi ya mwanasoka huyo.
Ikiwa ofa hiyo itafanikiwa, Sterling atakuwa mwanasoka anaelipwa zaidi chini ya kampuni ya PUMA na Kioo cha Matangazo yote ya Kimataifa ya kampuni hiyo ya kimataifa ya Ujerumani.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 kwasasa ana mkataba na Nike unaotarajia kuisha mwezi ujao (tarehe 30 June).
Sterling huenda akashirikiana kwenye ukuzaji wa brand ya Puma na rapper wa Marekani, Jay-Z, ambaye kwasasa ni mkurugenzi wa ubunifu wa kampuni hiyo.
Licha ya kuwindwa na makampuni mengine kama Adidas na New Balance, Sterling anaripotiwa kuwa karibu kusaini na Puma kutokana na kampuni hiyo kuwa na mkataba wa miaka 10 wenye thamani ya Pauni milioni 650 na klabu yake ya sasa Man City.



mathayo sonje
sterling anapiga bingo kiulaaiiiini kama kubashiri na meridianbet
Christopher
Huyu jamaa anazidi kupanda chart kadri Siku zinavyokwenda, ila hii ishu ya city kutokushiriki champions league inaweza kushusha status yake kisoka akiendelea kubaki city
Lombo
rahm yuko vizur chem achajiuza bhn
farida ahmadi
Hongera Raheem sterring
Furahav
Hongera