Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Diogo Jota amesaini kandarasi ya kuongeza muda wa kuitumikia klabu hiyo kwa miaka miwili zaidi ambapo kandarasi hiyo inatarajiwa kufika tamati mwaka 2027.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka ureno alijiunga na klabu ya Liverpool akitokea klabu ya Wolves kwa ada ya uhamisho inayokaribia £40million mwaka 2020, na kusaini kandarasi ya miaka mitano ambapo kandarasi yake ilikuwa inatarajiwa kuisha mwaka 2025.

“Ninajivunia kusema, bila shaka tangu nimewasiri miaka miwili iliyopita nijmeitengeneza kuwa mchezaji muhimu kwenye timu hii, hicho ndicho nilikuwa nahitaji tokea awali.

“Sasa nimesaini kandarasi ya muda mrefu, bila shaka haya maono ni uthibitisho wa klabu, ya kujiamini mwenyewe kama mchezaji. Kwangu ni vizuri kuwepo na nitakuwepo kwa muda. hivyo tunaanza msimu mpya, twende kazi.” Jota aliuwambia mtandao wa klabu.

Diogo Jota amefanikiwa kuichezea klabu ya Liverpool michezo 85 na kufanikiwa kufunga magoli 34 kwenye mashindano yote, pia amefanikiwa kuisadia klabu hiyo kuchukua ubngwa Carabao, FA Cup na kuifikisha fainali za ligi ya mabingwa ulaya msimu uliosha ambapo walipoteza dhidi ya Real Madrid.

Diogo Jota hakufanikiwa kusafiri na timu kwa ajiri ya michezo ya Pre-season kutokana na majeruhi lakini pia kuna wasiwasi pia anaweza kukosa ichezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya Uingereza wikiendi ijayo dhidi ya Fulham.


 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa