Diogo Jota Mchezaji Bora Mwezi Januari

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Ureno Diogo Jota amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi  Januari ya ligi kuu ya Uingereza akiwashinda wachezaji kadhaa ambao alikua anawania nao tuzo hiyo.

Jota amekua na wakati mzuri sana katika mwezi Januari kwani amecheza kwa kiwango bora na kusaidia klabu yake ya Liverpool kushinda alama katika michezo aliyocheza katika mwezi Januari.diogo jotaMshambuliaji huyo alikua anawania tuzo hiyo na wachezaji kadhaa kama Kevin de Bruyne kutoka Man City, Gabriel Magalhes kutoka Arsenal, Bradley kutoka Liverpool, Adebayo kutoka Luton Town, pamoja Richarlison kutoka Tottenham ila ni yeye ambaye ameweza kuinyakua tuzo hiyo.

Staa huyo wa Liverpool amekua na namba nzuri zaidi katika mwezi wa kwanza kuliko wenzake wote, Kwani alifanikiwa kuhusika kwenye mabao matano akifunga mabao matatu na kupiga pasi za mwisho zilizosaidia upatikanaji wa mabao mawili.diogo jotaKlabu ya Liverpool ilifanikiwa kukomba alama zote ambazo iliwania mwezi Januari huku mshambuliaji Diogo Jota akiwa na mchango mkubwa sana katika alama hizo, Ikiwa ndio sababu kubwa ya mchezaji huyo kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa mwezi Januari.

 

Acha ujumbe