Diomande Anavutia Wakubwa Tu Ulaya

Sakata la usajili wa Yan Diomande limekuwa gumzo kubwa, likihusisha majina makubwa ya soka barani Ulaya. Winga huyu wa RB Leipzig, ambaye anatambulika kama kipaji cha kisasa, sasa anavutia klabu kama Arsenal, Manchester City, Real Madrid na Liverpool.

Diomande Anavutia Wakubwa Tu Ulaya

Liverpool walikuwa wa kwanza kuweka mezani ofa ya €100m, lakini Leipzig waliikataa. Sasa Arsenal wanamwona kama mbadala wa Leandro Trossard, huku City na Madrid wakifuatilia kwa ukaribu. Hata hivyo, Paris Saint-Germain ndiyo ndoto ya Diomande. Tayari amekubaliana masharti binafsi na PSG kwa mkataba hadi 2031, lakini tatizo ni kwamba PSG bado hawajatoa ofa rasmi kwa Leipzig.

Leipzig wanashikilia msimamo, bei ya chini kabisa ni €120m. Hii inaleta mvutano, hasa baada ya mazungumzo ya awali kati ya Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi na boss wa Red Bull Oliver Mintzlaff wakati wa fainali ya Kombe la Dunia jijini New York.

Diomande Anavutia Wakubwa Tu Ulaya

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kikwazo kingine ni muundo wa dili. Leipzig wanataka kipengele cha loan-back ili Diomande abaki Ujerumani msimu mmoja zaidi, lakini kocha wa PSG Luis Enrique anapinga vikali. Anataka mchezaji apatikane mara moja ili kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kampeni za msimu mpya Ulaya.

Diomande Anavutia Wakubwa Tu Ulaya

Kwa sasa, hali ni ya kusisimua na yenye mvutano mkubwa. Diomande anaitaka Paris, Leipzig wanataka pesa na masharti yao, na wakubwa wa Ulaya wako tayari kuvunja rekodi. Sakata hili linaweza kuwa usajili mkubwa zaidi wa kiangazi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.