Novak Djokovic amekubali kipigo katika mchezo wa kwanza wa mashindano katika historia yake, ukosefu wa utimamu wa mwili ulimfanya kupoteza mchezo wa kwanza wa Monte Carlo Masters mbele ya Alejandro Davidovich Fokina.

 

Monte Carlo Masters.

Djokovic akicheza mechi yake ya pili tu mwaka huu, alifanya makosa 51 bila kulazimishwa katika mazingira magumu na kuambulia seti 6-3 6-7 (5-7) 6-1 katika raundi ya pili.

Djokovic alirejea kortini kwa mara ya kwanza tangu Dubai mnamo Februari, ambapo alipoteza katika robo-fainali dhidi ya Jiri Vesely. Bingwa huyo mara 20 wa Grand Slam alizuiliwa kucheza kutokana na vikwazo vinavyohusiana na hali yake ya chanjo ya Covid-19.

“Nimesikitishwa. Hakuna anayependa kushindwa. Sisi ni wachezaji wa kulipwa. Hiki ndicho tunachofanya. Tunaenda uwanjani kushindana na kujaribu kushinda dhidi ya kila mmoja,” Djokovic alisema.

 

“Sikupenda jinsi nilivyohisi kimwili katika seti ya tatu. Niliishiwa na pumzi kabisa. Sikuweza kuchuana nae. Ikiwa huwezi kushindana, kushindwa kuhisi miguu juu ya ardhi, ni jambo lisilowezekana.

 

“Sijapenda hisia hizo nilizozipata katika seti ya tatu lakini nitaangalia na timu yangu sababu kwa nini ilikuwa hivyo na matumaini yangu wiki ijayo itakuwa bora zaidi kule Belgrade.” aliongeza.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa