Fundi wa Tenisi, Novak Djokovic atavaana na mchezaji namba moja wa Uingereza, Cameron Norrie katika nusu fainali ya michuano ya tenisi ya Wimbledon.

Mchezaji wa Australia, Nick Kyrgios amepata mtelezo baada ya kutinga fainali ya michuano ya Wimbledon baada ya mchezaji namba moja wa dunia, Rafael Nadal kujiondoa katika nusu fainali baada ya kupata majeraha.

 

djokovic, Djokovic Kuvaana na Norrie Nusu Fainali ya Wimbledon., Meridianbet

Kyrgios alitinga nusu fainali hiyo baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Cristian garin kwa seti 6-4 6-3 7-6 (7-5) kabla ya mpinzani wake wa nusu fainali, Rafael Nadal kutangaza kupata majeruhi na kujiondoa katika mashindano ya Wimbledon.

Djokovic alipambana kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi katika hatu aya robo fainali ya michuano ya Wimbledon dhidi ya Jannik Sinner kwa seti 5-7 2-6 6-3 6-2 6-2.

Norrie anatarajia kupata chamoto ya kwanza kubwa dhidi ya Novak Djokovic baada ya kutinga katika nusu fainali hiyo. Mshindi katika fainali hiyo ataenda kuvaana na Nick Kyrgios.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa