Hapa tunakuletea dondoo kadhaa za usajili jumapili hii tarehe 26 Mei 2019.
Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri amekubali kuwa meneja anayefuata wa Juventus. Kwa mujibu wa chanzo cha Italia, meneja huyu anakubali ofa hii baada ya bosi wa Manchester City Pep Guardiola kukataa ofa hiyo.
Manchester City wanatarajia kumpatia ofa ya mshahara wa paundi 150,000 kwa wiki kwa nyota wa mjerumani Leroy Sane katika kuweka sawa ishu ya mkataba mpya na wanatarajia kuweka dau la ku8muuza nyota huyu kuwa paundi milioni 100. Nyota huyu wa miaka 23 anafukuziwa na Bayern Munich.
Manchester United wanatajwa kuwa wapo karibu zaidi kuinasa sahihi ya Matthijs de Light na kuwapiku Barcelona baada ya ofa nene. Hata hivyo mapenzi ya nyota huyu yako Barcelona licha ya dili analotajwa kupewa na Man Utd kuwa tamu na gumu kuliachia.
Chelsea wanadaiwa kuwa watahitaji Real Madrid wawalipe paundi milioni 130 kwa ajili ya uhamisho wa fowadi wa klabu hiyo Eden Hazard. Hata hivyo dondoo zinataja kuwa klabu ya Real Madrid inamuona staa huyu akiwa na thamani ya paundi milioni 88.
West Ham wanamuhitaji staa wa Barcelona mwenye miaka 25, Andre Gomes kwa dau la paundi milioni 18. Msimu uliopita kiungo huyu alitumika kwa mkopo na klabu ya Everton.
Staa wa Arsenal ambaye anamaliza mkataba wake klabuni hapo, Danny Welbeck, ambaye ana miaka 28 amewavutia klabu za Everton, Newcastle, West Ham na Lazio ambao wameunga tela kwenye mbio hizi za kuwania sahihi yake.
Meneja wa Benfica, Domingos Soares de Oliveira anasema Manchester United watatakiwa kulipa paundi milioni 105 kumsainisha kinda wa Benfica, mwenye miaka 19, Joao Felix.
Furahav
Mko vizuri.