Donnarumma: "Italia Iko Tayari kwa Mbinu Mpya"

Gianluigi Donnarumma anajiandaa kwa majaribio ya mbinu ya Italia dhidi ya Venezuela na Ecuador, kisha anakiri ‘kucheza na mpira miguuni mwako ni jambo la msingi’ sasa.

Donnarumma: "Italia Iko Tayari kwa Mbinu Mpya"

The Azzurri itamenyana na Venezuela huko Fort Lauderdale Alhamisi, kisha Ecuador siku ya Jumapili katika uwanja wa Red Bull Arena huko New Jersey.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Haya ni baadhi ya majaribio ya mwisho ya kirafiki ambayo yameandaliwa kabla ya michuano ya Euro 2024 kuanza mwezi Juni.

Donnarumma aliiambia Sky Sport Italia, “Lazima tujiandae kwa Euro kwa umakini, michezo yote ni muhimu”

Donnarumma: "Italia Iko Tayari kwa Mbinu Mpya"

Kocha Luciano Spalletti alisema atatumia mechi hizi kufanya majaribio ya kimbinu. Bila kujali mfumo tunaotumia, kocha ataamua, tunatakiwa kuwa tayari. Ikiwa kuna hitaji, tunaweza kucheza na watatu nyuma, vinginevyo tutacheza na wanne. Alisema kocha huyo.

Golikipa huyo anasema kuwa, kucheza na mpira miguuni ni jambo la msingi kwa soka la kisasa. Wanatayarisha kila mechi kwa njia sahihi ili kuwa na uwiano wa kimbinu na nafasi kubwa ya kuwaumiza wapinzani wao.

Kipa huyo wa zamani wa Milan pia alizungumza na chaneli rasmi za mitandao ya kijamii za FIGC.

“Tunacheza timu mbili ngumu za Amerika Kusini, kwa hivyo tunahitaji kujiandaa vyema na kukabiliana nazo kwa njia bora. Hata kama ni za kirafiki, kuzichezea kwa mawazo sahihi kutatuweka katika hali nzuri zaidi kwa mechi zijazo.”

Donnarumma: "Italia Iko Tayari kwa Mbinu Mpya"

Ni mara ya kwanza kwa Italia kucheza nchini Marekani kwa miaka 19 na michezo hii iliandaliwa kwa ajili ya jamii ya Waitaliano na Marekani.

Bingwa wa tenisi Jannik Sinner alitembelea uwanja wa mazoezi huko Miami jana na kupiga picha na wachezaji wa Azzurri.

Nimemfahamu kwa muda, ni rafiki na tunazungumza mara kwa mara. Anaweka mfano kwa michezo yote ya Italia, tunajivunia kile anacholeta Italia na tunamtakia kila la kheri kwa siku zijazo. Tunatumai kupitisha baadhi ya mawazo yake na hamu ya kushinda. Alimaliza hivyo kipa huyo.

Acha ujumbe