Kiungo wa klabu ya Manchester United Donny Van de Beek hajaorodheshwa kwenye kikosi cha klabu hiyo kitakachoshiriki mihuano ya ligi ya mabingwa ulaya msimu huu.
Kiungo Donny Van de Beek amekua akihusishwa kuondoka ndani ya klabu hiyo haswa klabu ya Real Sociedad ya nchini Hispania, lakini ilishindikana kuondoka klabuni hapo kwenye majira haya ya kiangazi.Manchester United hawajamjumuisha kiungo huyo kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya ulaya msimu huu, Huku ikiaminika huenda klabu hiyo haijaamua kumjumuisha kiungo huyo kwasababu bado inataka kumuachia mchezaji huyo.
Kiungo Donny Van de Beek amekua na wakati mgumu tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2020 kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara, Majeraha pia ndio yanaonekana kupoteza nafasi yake kabisa kwenye timu hiyo na haishangazi kuonekana hayupo kwenye mipango ya timu hiyo.Klabu ya Manchester United mbali na kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi lakini timu hiyo pia haijamjumuisha winga Alejandro Garnacho katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, Lakini kwa Garnacho inaelezwa atatoka kwenye orodha ya pili na atashiriki michuano hiyo.