Klabu ya Borrusia Dortmund inalenga kuwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Bundesliga ambapo itashinda mchezo wao wa leo ambao watakuwa ugenini kukipiga dhidi ya RB Leipzig ambaye hana matokeo mazuri toka kuanza kwa msimu huu.

 

Dortmund Yalenga Nafasi ya Kwanza

Msimamo wa Bundesliga unaanza kuimarika taratibu, na kuteleza kwa miamba wa Ujerumani Bayern Munich katika mechi mbili zilizopita kwa kutoa sare kumewapa wapinzani wao nafasi ya kusonga mbele.

Borrusia Dortmund watakuwa na nia ya kuweka pua zao mbele ya Bayern lakini inabidi wakabiliane kwanza na Red Bull Salzburg. Lakini mabingwa hao watetezi wa ligi watajiamini kwurejea uwanjani baada ya sare waliyoipata ya 1-1 dhidi ya Union Berlin.

 

Dortmund Yalenga Nafasi ya Kwanza

Na kwa upande wa viongozi wa ligi hiyo Freiburg wao watacheza dhidi ya Borrusia Monchengladbach. Dortmund msimu uliopita alipigwa nje ndani na RB Leipzig na kupoteza jumla ya mabao 6-2.

RB Leipzig ambayo imemuajiri kocha wa zamani wa dortmund Marco Rose atakuwa akikabiliana na waajiri wake wa zamani baada ya kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha klabuni hapo  Tedesco japokuwa ana kibarua kizito kinachomkabili mbele yake.

 

Dortmund Yalenga Nafasi ya Kwanza

Leipzig wanastahimili mwanzo wa wa pili mbaya ziadi kuwahi kutokea Bundesliga, wakivuna alama tano tuu katika michezo yao mitano ya kwanza na kupoteza mchezo wao wa mwisho wdhidi Frankfurt kwa mabao 4-0. Wakati kwa upande wa Dortmund wao wakiwa wameshinda mechi zao nne na kupoteza moja wakiwa na alama 12.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa