Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube yuko fiti kucheza mechi zilizosalia ikiwemo ya nusu fainali dhidi ya Simba licha ya juzi kushindwa kuendelea na mchezo.
Ilimchukua dakika sita tu ambazo Dube alizitumia katika mchezo wa juzi kabla ya kutolewa kutokana na maaumivu makali ya tumbo yaliyomkumba ghafla.
Akizungumza hali ya Dube Ofisa habari wa Azam, Thabit Zakaria amesema mchezaji huyo yupo vizuri na jana hakuumia bali alipata maumivu ya tumbo yaliyosababisha kutoendelea na mchezo.
Amesema ilitokea ghafla mchezaji huyo alijisikia maumivu makali ya tumbo na kuomba atolewe lakini kwa sasa yuko vizuri.
Zakaria amesema wamerudi Dar es Salaam tayari kwa maandalizi ya michezo ijayo ikiwemo wa nusu fainali dhidi ya Simba na mechi za Ligi Kuu zilizosalia.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.
Habari njema kwa mashabiki wa azam
Dube ni mchezaji anayefaa kuigwa na wachezaji wetu wa ndani, Ni wakati sasa na sisi wazawa tukaamka kufanya kweli katika soka ata katika nchi za watu
Habari nzuri
Itakuwa bonge la mchuano
Full shangwe kwa Azam