Mshambulizi wa Fiorentina Dusan Vlahovic ameripotiwa kufikia makubaliano binafsi na Juventus kabla ya kukamilisha uhamisho na wababe hao wa Serie A.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ni mmoja wa washambulizi wanaosakwa sana barani Ulaya, huku Arsenal ikiaminika kuwa inaongoza katika mbio za kuwania saini yake.
Hata hivyo, mwanahabari wa Italia Giacomo Scutiero anadai kuwa The Gunners hawana nafasi ya kumpata Vlahovic, kwani tayari alikubali kujiunga na Juventus mwezi Oktoba.
Scutiero pia anasema kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia ndiye mchezaji pekee ambaye Juventus wamejiandaa kumsajili kwa pesa nyingi mwezi huu au majira ya joto, huku mchezaji mwenyewe akiwa na nia ya kusajiliwa na klabu hiyo hata kama watashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Kocha mkuu wa Fiorentina Vincenzo Italiano anaamini Vlahovic ‘anaendelea kuwa na ari ya kuichezea klabu hiyo ingawa mshambuliaji huyo amebakiza chini ya miezi 18 tu kwenye mkataba wake.
Vlahovic alifunga bao lake la 17 la Serie A msimu huu katika ushindi wa bao 6-0 dhidi ya Genoa Jumatatu, jambo ambalo linamfanya awe sawa na Ciro Immobile wa Lazio kileleni mwa msimamo wa mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu.
Manchester City, Manchester United, Tottenham Hotspur na Real Madrid pia wametajwa kuwa na nia pia ya huduma ya Vlahovic.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA