Dyabala Ameichomoa United

Klabu ya Juventus imeamua kuja juu na kujibu tetesi zinazomuhusisha nyota wao Paul Dyabala kuhamia klabu ya Manchester United.

Siku za hivi karibuni nyota huyu amekamata vichwa vya habari vya vyanzo mbali mbali vya habari za michezo kuwa anatarajiwa kuhamia Old Trafford.

Licha ya kuthibitisha kuwa Massimiliano Allegri anasepa klabuni hapo, klabu hii inasisitiza kuwa Dyabala anabaki kuwa mchezaji muhimu kwa klabu hiyo.

Mkurugenzi wa michezo Fabio Paratici anasisitiza kuwa nyota huyu anabaki kuwa sehemu muhimu ya timu bila kujali ni nani atakayechukua madaraka ya meneja msimu unaofuata.

“Ni mchezaji wetu, tunamumini sana. Kwa pesa tulizowekeza kwake kwa miaka minne na kuongeza kwake kwa mkataba ni uthibitisho tosha wa hili. Dyabala ni mchezaji wa Juventus, mchezaji muhimu sana kwetu.”

Hata hivyo, nyota huyu pia anataka kusalia klabuni hapo, akizungumzia kuhusu adhma yake hiyo

“Paratici anatambua nini nahitaji kufanya mwakani nataka kubakia hapa. Juventus wanatakiwa kufanya maamuzi yao kuhusu meneja anayekuja. Lakini jamii inatambua kuwa nahitaji kusalia hapa mwakani”

2 Komentara

    Bora asiende tu

    Jibu

    asante kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe