Nyota wa Juventus Paul Dybala ameripotiwa kusafiri kwenda Barcelona kwa ajili ya kuonana na mtaalamu wa matibabu ya goti huko Hispania Ramon Cugat.

Staa huyu ameamua kufunga safari yake kwa ajili ya kujadili suala la jeraha lake la goti ambalo limekuwa likimsumbua na kuathiri ushiriki wake kwenye mechi.

Nyota huyu wa miaka 27 ameshindwa kuhusika na michezo mingi ya kuanzia mwezi Januari kwa sababu ya jeraha hilo, na alihitaji zaidi kufanyiwa matibabu ya uhakika, na kwa mujibu wa Goal  Dybala ameamua kufanya safari kwenda Hispania.

Mkurugenzi wa Juventus amethibitisha pia kuwa suala la hatma ya staa huyo klabuni hapo lina walakini kidogo kutokana na kusuasua kwa mazungumzo ya mkataba mpya.

Dybala amesalia na takribani miezi 18 kwenye mkatana wake wa sasa na vilabu vya Liverpool, Manchester United na Tottenham Gotspurs vinatajwa kuwa vinavutiwa na huduma yake na vinalenga kuinasa saini yake.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

Dybala, Dybala Asafiri Kwenda Barcelona, Meridianbet

CHEZA HAPA

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa