Dylan Kerr aliyewahi kuinoa Klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara amepewa kibarua cha kuinoa timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Kerr mwenye miaka 53 ana uzoefu na soka la Afrika kwa kuwa aliwahi kuinoa Klabu ya Baroka FC msimu wa 2020 ambapo aliibuka ndani ya klabu hiyo akitokea Klabu ya Black Leopards.
Pia aliwahi kuifundisha Klabu ya Gor Mahia msimu wa 2017/18 nchini Kenya baada ya kuchimbishwa ndani ya Simba aliyoifundisha msimu wa 2015/16.
Black Leopards imemrejesha tena Kerr ndani ya kikosi hicho baada ya kumfuta kazi Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ambaye naye aliifundisha Simba kwa msimu wa 2019/20 na aliweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara.
Akiwa ndani ya timu hiyo alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi tatu na zote alipoteza jambo ambalo limewafanya mabosi wa timu hiyo kumfuta kazi jumlajumla.
Habari kutoka Afrika Kusini zimeeleza :”Kerr atafanya kazi na Morgan Shivambu na Mongezi Bobe akichukua mikoba ya Aussems,” ilieleza taarifa hiyo.
Ndani ya Baroka FC, kocha huyo alifutwa kazi hivyo anarejea kwenye timu yake ya zamani akiwa huru.
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.
magdalena
pongezi kubwa sana kwake akapige kazi sasa
Fatina mfingi
Kapige kazi ss ujue umepewa dhaman kubwa!
Sadick
Kuna haja kubwa kukuza Makocha wazawa kuliko hawa wanazunguka kila Klabu na kufanya kazi muda mfupi na kufukuzwa kisha kuajiriwa tena Klabu nyingine
Ester jackson
Wazawa kwanza ingawa frusa hizi hazipatikani kwa wepisi wanapata wageni na mwishowe wakiharibu tu wanaondolewa
Sauda
Piga kazi kijana
Mariam mtandama
Habari njema
Issa
Mtu wa kaz
zeiyana
Dylan kerr mda wake sasa wa kufukia makosa yake
Rahma
Kazi kaz piga kaz
Lydia Emmanuel Magoti
Kazi nzuri kijana piga kazi
Ernest
Gundu linaendelea kwa Aussems
felister
piga kazi
Tahiya
Maskini uchebe sijui anakwama wapi nako kafukuzwa
Caroline
Hongera
Adelta
Kijana Yuko vizuri apige kazi
Fatuma kasomo
Piga kazi
Hopemwaikuka
Jambo zur hili
Saupha mohamed
Jmaa yupo vizuri
Povel
Uchebe zimu la msimbazi bado linamtafuna
warda
hongera yake