Wachezaji wa Manchester City Earling Haaland na Phil Foden wamepiga hat-trick kila mmoja katika mchezo wa Manchester Derby ambao klabu ya Man City imetoa kipigo cha aibu kwa klabu ya Man United cha mabao sita kwa matatu.
Mchezaji Earling Haaland amekua na kiwango bora sana katika mchezo huo baada ya kufunga magoli matatu na kupiga pasi mbili za mabao huku Phil Foden nyota huyu wa kiingereza akifunga magoli matatu na kupiga pasi moja ya bao.
Wachezaji hao wameweza kutakata katika mchezo huo ambao ulionekana umeelemea upande mmoja baada ya klabu ya Man City kwenda mapumziko wakiongoza magoli manne kwa bila kabla ya kuongeza magoli mawili kipindi cha pili huku United wakipata magoli matatu na kufanya mchezo kumalizika kwa mabao sita kwa matatu.
Earling Haaland sasa anafikisha magoli 14 katika mechi 8 za ligi kuu Uingereza huku akiwa na mabao 16 katika michuano yote na kuendelea kudhihirisha ubora wake kwa wale ambao walimtilia mashaka hapo awali.
Klabu ya Manchester City City inaendeleza rekodi yake ya kutopoteza mchezo katika nane iliocheza mpaka sasa huku ikiwa imesuluhu michezo miwili na kushinda sita na kukusanya alama 20 huku ikiwa nyuma kwa alama moja dhidi ya klabu ya Arsenal vinara wa ligi hiyo.