Nyota wa Real Madrid, Eden Hazard amewaahidi klabu yake kuwa msimu ujao 2022/23 atafanya makubwa zaidi.

Nyota huyu mwenye uraia wa Ubelgiji amekuwa akisumbuliwa na shida ya majeraha tangia alipowasili Hispania mwaka 2019 akitokea Chelsea.

kwa ujumla staa huyu amekosa michezo takribani 72 ya Real Madrid kwa michuano yote, tangia mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 akiwa amecheza mechi 48 pekee za La Liga.

Msimu wa 2021/22 staa huyu ameweza kucheza mechi saba pekee.

Hakuingia dimbani kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool jumamosi, walipoibuka na ubingwa, lakini amesisitiza kuwa msimu ujao anataka kuwapa furaha mashabiki wa Madrid.

“Madristas, nimekuwa hapa kwa miaka mitatu nikipata majeraha mengi… lakini msimu ujao ninaenda kuwapa kila kitu” – Eden Hazard

Bosi wa Real Madrid, Carelo Ancelotti ameweka wazi nia yake ya kuutaka kusalia na staa huyu akiamini kuwa suala lake la majeraha linaisha na atakuwa bora.

Real Madrid


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa