Golikipa wa klabu ya Manchester City Ederson Moraes amefanikiwa kuweka rekodi ya kufikisha michezo 100 kwenye ligi kuu ya Uingereza bila kuruhusu wavu wake kuguswa.
Ederson ambaye kwasasa ana msimu wa sita ndani ya klabu ya Manchester City kwani golikipa huyo alijiunga na klabu hiyo mwaka 2017 akitokea klabu ya Benfica ya nchini Ureno, Amefanikiwa kuweka rekodi hiyo baada ya kucheza misimu sita ndani ya klabu hiyo kutoka jiji la Manchester.Golikipa huyo wa kimataifa wa Brazil licha ya kufikisha michezo 100 bila kuruhusu wavu wake kuguswa lakini amekua moja ya magolikipa bora sana katika ligi kuu ya Uingereza tangu atue klabuni hapo, Kwani katika kudhihirisha hilo golikipa huyo amefanikiwa kushinda tuzo ya golikipa bora mara tatu.
Ederson amefanikiwa kutwaa tuzo ya golikipa bora wa ligi kuu ya Uingereza mara tatu katika misimu ya 2019/20, 2020/21, 2021/22 ikiwa inaonesha namna gani amekua bora kwenye misimu sita ambayo amecheza mpaka sasa amefanikiwa kua golikipa bora wa ligi hiyo mara tatu.Ederson Moraes pia amefanikiwa na klabu ya Manchester City licha ya mafanikio yake binafsi kwani golikipa huyo amefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Uingereza mara nne tangu atue klabuni hapo, Fainali ya michuano ya Uefa mwaka 2021, taji la Fa Cup mara moja, Vilevile wakifanikiwa kushinda taji la Carabao mara nne.