Golikipa namba moja wa klabu ya Manchester City raia wa kimataifa wa Brazil Ederson Moraes ana hatihati ya kutimka ndani ya klabu hiyo mabingwa wa Uingereza.
Ederson inaelezwa yupo kwenye kwenye mazungumzo na vilabu kadhaa kutoka nchini Saudia Arabia ambapo inaelezwa wamempa ofa kubwa golikipa huyo, Hivo inaelezwa kua nyanda huyo amevutiwa na ofa hizo na inawezekana kwa kiwango kikubwa atatimka klabuni hapo.Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi bado hajajua kama golikipa huyo ataendelea kusalia ndani ya klabu kuelekea msimu ujao, Kauli ya Guardiola imeonesha wazi kua kuna asilimia kubwa kwa golikipa huyo kutimka ndani ya timu hiyo kuelekea msimu ujao.