Ederson: Vini Anastahili Kushinda Ballon Dor

Golikipa wa klabu ya Manchester City Ederson Moraes raia wa kimataifa wa Brazil amesema kua winga wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania Vinicius Jr anastahili kutwaa tuzo ya Ballon Dor kwa mwaka 2024.

Ederson ameyasema hayo wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Brazil wakijiandaa kucheza mchezo wa kufuzu michuano ya kombe la dunia mwaka 2026, Ndipo golikipa huyo aliweka wazi kua winga huyo ambaye anacheza nae timu ya Brazil Vinicius Jr anastahili kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.ederson“Natumaini Viní Jr atashinda Ballon d’Or.”

“Anastahili kwa kila kitu alichofanya msimu uliopita. Kwa upande mwingine, kama Rodri akishinda nitafurahi pia.”

Golikipa Ederson ametupiwa maneno na mashabiki wa klabu yake ya Manchester City wakidai alitakiwa kumuunga mkono mchezaji mwenzake wa klabu hiyo Rodri ambaye na yeye yupo kwenye nafasi nzuri ya kushinda tuzo hiyo, Lakini badala yake amempa nafasi Vinicius ikumbukwe Vinicius pia ni mchezaji mwenzake wa timu moja kwa upande wa timu ya taifa na ndio sababu kubwa ya golikipa huyo kumuunga mkono winga huyo.

Winga Vinicius Jr amekua na msimu bora sana uliomalizika na kufanikiwa kufanya mambo makubwa mpaka sasa kuzungumzwa kama mchezaji ambaye anapewa nafasi kubwa zaidi kutwaa tuzo ya Ballon Dor mwaka 2024, Huku akiwa na washindani wa karibu kama Bellingham ambaye ni mchezaji mwenzake klabuni, Rodri, pamoja na mchezaji Dani Carvajal anayekipiga klabu ya Real Madrid.

Acha ujumbe