Eguavoen Ajiuzulu Baada ya Nigeria Kung'olewa AFCON 2021.

 

Kocha wa muda wa timu ya Taifa ya Nigeria, Augustine Eguavoen ameandika barua rasmi ya kujiuzulu mara moja nafasi ya Ukocha Super Eagles baada ya kuondoshwa Jana dhidi ya Tunisia.

 

Augustine Eguavoen

Hatua hii inakuja muda mchache baada ya Super Eagles kupoteza 1-0 dhidi ya Tunisia katika mchuano wa hatua ya 16 bora wa Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 mnamo Jumapili.

Eguavoen alikuwa ameongoza mabingwa hao mara tatu kwa ushindi mara tatu mfululizo dhidi ya Misri, Sudan na Guinea-Bissau katika hatua ya makundi.

“Kinachotokea baadaye ni kwamba mimi ni kocha wa muda na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF).

“Nitarejea kwenye msimamo wangu na kuruhusu NFF (kufanya) uamuzi kuhusu njia ya kusonga mbele,” kocha huyo alisema baada ya mechi.

Eguavoen aliingia madarakani baada ya Gernot Rohr kufutwa kazi mwezi uliopita. Hata hivyo, NFF ilimtangaza Jose Peseiro kuwa kocha mpya wa kudumu kabla ya AFCON 2021 kuanza.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe