Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na raia wa kimataifa wa Sweeden Anthony Elanga anaisubiri klabu yake iweze kumpa ruhusa ili aweze kujiunga na Borussia Dortmund.
Mshambuliaji huyo anahitaji kuondoka ndani ya klabu ya Manchester United kwa mkopo kuelekea klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya Ujermani. Mchezaji huyo ameamua kufanya uamuzi huu ili aweze kupata muda wa kucheza zaidi.Klabu ya Manchester United ipo kwenye mpango wa kuwaachia baadhi ya wachezaji wake kwenda kwa mkopo ili waweze kupata nafasi nje ya klabu hiyo, Anthony Elanga ni miongoni mwa wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo katika dirisha hili la mwezi Januari.
Anthony Elanga ameonesha matamanio makubwa ya kujiunga na klabu ya Borussia Dortmund katika dirisha hili dogo, Huku yeye akiwa anasubiri taarifa ya mwisho ya klabu yake kumruhusu kujiunga na klabu baada ya kumalizana na Borussia Dortmund.Anthony Elanga ataungana na kinda mwingine ndani ya klabu ya Manchester United kuondoka klabuni hapo kwenye dirisha dogo la mwezi Januari, Wakienda nje ya klabu hiyo ili kupata nafasi ya kucheza zaidi na kupata uzoefu nkwenye vilabu ambavyo wataelekea.