Kinda wa Tennis Uingereza, Emma Raducanu, 19 amejiondoa katika michuano ya Tennis ya Dunia ya Mubadala baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Raducanu ambaye ni mshindi wa US Open, tayari amesafiri kuelekea umoja wa nchi za kiarabu (United Arab Emirates) kwaajili ya mashindano hayo wakiwemo Andy Murray na Rafael Nadal.
Kinda huyo alitakiwa kukutana na mshindi wa Olympic, Belinda Bencic katika jiji la Abu Dhabi siku ya Alhamisi.
“Nilikua nimejiandaa kucheza mbele ya mashabiki zangu hapa Abu Dhabi, lakini bahati mbaya baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona, imebidi nihairishe mpaka nafasi nyingine tena,” alisema Raducanu
“Nimejitenga kama sheria zinavyotaka na natumaini nitarejea mapema uwanjani.” aliongeza.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.