Enrique Amtema Donnarumma, Kuwindwa na Man City na United

Kuelekea fainali ya UEFA Super Cup usiku wa leo nchini Italia, kocha wa Paris Saint-Germain, Luis Enrique, amethibitisha kwa sauti yake mwenyewe kuwa uamuzi wa kumtema Gianluigi Donnarumma kwenye kikosi ulikuwa wake binafsi na yuko tayari kubeba lawama zote.

Enrique Amtema Donnarumma, Kuwindwa na Man City na United

PSG, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, wanakabiliana na Tottenham Hotspur bila kipa wao namba moja kwa misimu minne. Mkataba wa Donnarumma unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hali inayomweka katika nafasi ya kuondoka bure kama haitaafikiwa dili jipya.

“Tension imetanda. Gigio ni mmoja wa makipa bora duniani na ni mtu bora zaidi,” Enrique aliiambia Sky Sports Italia. “Lakini maisha ya soka yako hivi na hivyo ndivyo ilivyo kwa makocha pia. Huu ni uamuzi mgumu, na ninachukua jukumu lote. Ni uamuzi unaohusu aina ya kipa ninayehitaji kwa timu yangu.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Enrique Amtema Donnarumma, Kuwindwa na Man City na United

Nafasi ya Donnarumma itachukuliwa na Lucas Chevalier, sajili mpya wa PSG kutoka LOSC Lille kwa dau la takribani €40 milioni wiki iliyopita.

Ripoti kutoka RMC Sport zinaeleza kuwa Manchester City wamemweka Donnarumma kama chaguo lao kuu endapo Ederson ataondoka Etihad baada ya miaka nane aliyohudumu hapo. Vyombo vya habari vya Uturuki vimeongeza kuwa Galatasaray pia wameonyesha nia.

Hata hivyo, ingawa Manchester United wametajwa na vyanzo kadhaa, Daily Mail inadai uhamisho huo haupo karibu kutokea, huku Manchester Evening News ikiripoti kuwa Ruben Amorim anataka kipa mpya, lakini hakuna bajeti rasmi iliyowekwa kwa sasa.

Enrique Amtema Donnarumma, Kuwindwa na Man City na United

Kwa sasa, macho yote yameelekezwa Italia, je, PSG itaweza kuanza msimu kwa taji kubwa bila ngome yao ya muda mrefu golini? Wakati huo huo, soko la usajili linaanza kuwaka moto kwa jina la Donnarumma.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.