Enzo Fernandez Awaomba Radhi Wenzake

Kiungo wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Argentina Enzo Fernandez amerejea kwenye kikosi cha klabu hiyo kilichopo nchini Marekani kwajili ya kujiandaa na msimu mpya.

Enzo Fernandez baada ya kufika kambini kwenye kikosi cha klabu yake ya Chelsea alilazimika kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake kikosini baada ya tukio alilolifanya akiwa na timu yake ya taiafa ya Argentina ambalo lilikua likiashiria vitendo vya ubaguzi kwa mchezaji wa kimatiafa wa Ufaransa Kylian Mbappe.enzo fernandezKufuatia video hiyo iliyosambaa wiki kadhaa zilizopita iliibua hisia miongoni mwa wachezaji wenye asili ya Afrika kwenye kikosi cha Chelsea na kupelekea kuzua taharuki klabuni hapo, Jmabo ambalo lingeweza kuleta mpasuko mkubwa ndani ya kikosi chao na kiungo huyo kulazimika kuomba msamaha ili kuweka mambo sawa.

Nahodha wa klabu hiyo Reece James pamoja na beki Axel Disasi ndio wanaelezwa walisimamia zoezi zima la kiungo Enzo Fernandez kuomba msamaha wachezaji wenzake ndani ya kikosi, Huku akiahidi atakua mstari wa mbele kuhakikisha anatokomeza suala la ubaguzi kwakua yeye atakua balozi mzuri wa kupinga vitendo hivyo.

Acha ujumbe