EPL: Kughairisha Mchezo, Sababu Ni....

Kumekuwa na hali ya sintofahamu miongoni mwa wachezaji, makocha na mashabiki wa EPL, hii ni kutokana na maamuzi ya kughairisha michezo ya ligi.

Uongozi wa EPL unanyooshewa vidole na wadau wakitaka uwazi kwenye sheria zinazotumika kughairisha michezo ya Ligi soka nchini Uingereza. Kwa sasa, imekuwa kama ni tamaduni kusikia mchezo fulani umeghairishwa.

Pengine kuna kitu kinafanyika nyuma ya pazia, mimi na wewe hatujui. Kuelekea muendelezo wa Premier League wikiendi hii, mchezo wa Burnley vs Leicester City umeghairishwa huku ikiripotiwa kuwa, Arsenal wameuomba uongozi wa Ligi hiyo kughairisha mchezo wao dhidi ya Tottenham Hot Spurs.

Kumekuwa na mvutano miongoni mwa makocha wa vilabu vinavyocheza ligi hiyo, baadhi yao wakihoji sababu kuu inayopelekea michezo kughairishwa ni ipi – Je, ni COVID19? Majeruhi? au uhaba wa wachezaji vilabuni (wanaoshiriki AFCON)?

EPL

Hakuna mwenye majibu sahihi katika hili. Japokuwa, makocha wamekuwa wakinyoosheana vidole wenyewe kwa wenyewe kwa kutaka uwazi kwenye idadi ya wachezaji walioathirika na COVID-19 kwenye vikosi vyao.

Siku kadhaa zilizopita, EPL walisema hadharani kuwa, msimu wa 2021/22 hautosimamishwa kwa misingi ya maambukizi ya COVID-19. Lakini, watakuwa wakiamua mchezo upi usimame kwa sababu hizo kulingana na hali halisi ya vikosi vya timu husika.

Kutokuwa na uwazi katika maamuzi, kunapelekea baadhi ya makocha na wadau wa mchezo kuwa na walakini kwenye michezo inayoghairishwa huku kukiwa na hisia kwamba, huenda kuna janja janja kwa baadhi ya vilabu kutaka kujiwekea idadi kubwa ya viporo kwa maslahi binafsi.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe