Erasto Nyoni Watu wamezaliwa, wamemkuta na bado wamemuacha. Nani huyo? Fungua mdomo kisha tamka kwa heshima jina lake,

Kama upo na afande hapo karibu, msogezee simu muoneshe picha ya Erasto Nyoni kisha muambie huyu ni askari mwenzako ila kazi zake anazifanya uwanjani zaidi kama utaona kheri basi mpigie saluti.
Miaka zaidi ya kumi na mbili anasimama dimbani mtulivu kama mtungi wa maji. Katika misukosuko na nyakati ngumu kiwanjani Erasto hataondolewa na tabu ya mchezo.
Miaka zaidi 30 duniani lakini bado mpya kama ameanza jana tu. Mti mkavu huu unaostahimili masika na kiangazi, na bado unasubiri mabadiliko mengine ya tabia ya nchi.

Timu ya taifa na jezi yake namba nne kifuani bado Erasto kama ameanza juzi tu. Katikati hapa alitaka kustaafu lakini taifa lilipinga, muhimu huyu kama oxygen kwa binadamu.
Katikati hapa alienda na Simba robo fainali ya Afrika, kwenye ukuta yeye na Pascal Wawa Sergie wa Ivory Coast waliiweka Simba salama mbele ya washambuliaji hatari Afrika.
Yeye kama James Milner wa Uingereza, muite tu naye ataitika. Mchezeshe beki, mchezeshe kiungo, mchezeshe kulia au kushoto ataitika siku zote. Wala hautakuwa na mashaka, atakupa unachotaka.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.