Erasto Nyoni, Kuzeeka ni Hiari

Hodi hodi jijini San Joaquín nchini chile yalipotimu mazazi ya Arturo Vidal, nyinyi mna nyota yenu, sisi tuna bahati yetu. Hodi tena kinshasa ya congo, hapo alizaliwa Claude Makélélé, Kiungo bamia, ni nuru ile, hodi tena hapo Sao Paulo Brazil, nyie mlimkuza Roberto Carlos wenu, nasi tuna jiji letu linaitwa Dar es salaam, nasi tukamkuza Erasto Nyoni.


.
Wala msitutishe na tambo zenu, nasi tunalo la kujigamba, Mjasiriamali mmoja huko marekani Mr Walt Disney aliwahi kusema “Growing old is mandatory, but growing up is optional!” (Kuzeeka ni lazima, lakini kukua ni hiari). Erasto wetu ameyageuza maneno haya, kwake yeye kukua ni lazima, kuzeeka ni hiari. Nyoni ndio mtungi wa soka huku kwetu. Mpira hutulia kama anavyouamuru.
.
Bado nipo na nyinyi watu wa kusini, sitomsahau yule Arturo Vidal wa 2015 pale Estadio Nacional Julio Martinez, fainali ya COPA AMERICA, dakika 90 za damu zinamalizika kwa 0-0, kisha penati zinaamua Chile Achukue ubingwa. Vidal anaibuka Man of the match, alijitoa sana siku ile, ni kama alikunywa maji ya bendera, hii ndio haiba ya Nyoni anapovaa jezi ya Taifa stars na simba.


.
Juzi tu mwalimu Didier Gomez alimualika bwana Erasto pale jijini Khartoum Sudan, walipo sare na El Merikh, anatoka mzamiru anaingia Nyoni, kisha kilichofuata ni historia tu, alimiliki dimba mithili ya Claude Makelele pale darajani The blues.
.
Bado nipo nanyi watu wa kusini mwa amerika. Ile ladha ya Roberto Carlos pale Inter Milan 1995–1996, imehamia Mo simba Arena kisha inaoneshwa kwa mkapa. Si mwingine ni Mwana wa Edward Nyoni, anayetuma na ya kutolea. Hivi sasa yupo na Kim Poulsen akipasha kuwakabili Equatorial Guinea. Bado tunaenjoy soka lake, kadri anavyokua ndiyo anazidi kuwa mtamu.


.
Nyoni ni kiraka chenye nidhamu, kila sehemu kinakaa tena kwa heshima ya soka, hivi sasa anazigawa busara kwa Nondo Mwamyeto na nduguye Abdallah Sebo, kisha anauchanga upatu kwa kelvin Cotton Yondani, taifa letu lipo salama sana enyi Watu wa kusini.


Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.

Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Imeeleweka

    Jibu

    Kweli kabisa

    Jibu

    Iko poa

    Jibu

    Kumbe

    Jibu

    Erasto yupo vizuri

    Jibu

    Ni kweli kabisa maneno ya Erasto nyoni

    Jibu

    Yuko sawa

    Jibu

    Bado yupo vizuri

    Jibu

Acha ujumbe