Kocha wa Manchester Eric Ten Haag amesikitishwa na kikosi chake kutojiamini katika mchezo dhidi ya klabu ya Manchester City baada ya kupoteza kwa magoli sita kwa moja.

eric ten haagEric Teb Haag anaamini vijana wake walionesha unyonge kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo huo na kueleza walikua na ari kwa wiki kadhaa nyuma lakini hali hiyo wameshindwa kuileta uwanjani leo dhidi ya City “Nimeshngaa kwanini hatukuileta uwanjani. Nimeona kwa winne tofauti timu tofauti,roho tofauti,mchezo wa tofauti na kiwango cha kujituma tofauti”.alisema Eric Ten Haag

“Leo hatukujituma. Kuanzia dakika ya kwanza ya mchezo hatukuanza kwa kujiamini,pia hatukua na ujasiri kumiliki mpira”Nitazungumza na wachezaji wangu ili kujua, wanajua walicheza vizuri dhidi ya Liverpool na Arsenal na kujituma sasa kama hutapambana kwa timu kama City ni tatizo”alisema Eric ten haag

eric ten haagBaada ya kupoteza mchezo huo kocha huyo anaungana na watangulizi wake David moyes,Luis Van gaal, Jose mourinho,Ole gunnar solskjaer, pamoja na Ralf rangnick kutokushinda michezo yao ya kwanza ya ligi kuu ya uingereza dhidi ya City.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa