Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag amesifu ubora wa nyota wa klabu hiyo baada Marcus Rashford baada ya kuulizwa swali kuhusu mchezaji huyo.

eric haagEric Ten Haag amesema hayo baada ya kuulizwa kuhusu nyota huyo katika mahojiano aliyoyafanya kuelekea mchezo wa dabi siku ya Jumapili, Kocha huyo amefunguka kuhusu tetesi zilizokua zinamuhusisha nyota huyo kujiunga na klabu ya PSG na kupiga na klabu hiyo kukataa kumuuza mchezaji huyo kuelekea kwa mabingwa hao wa Ufaransa.

Kocha huyo ameeleza toka amefika siku ya kwanza klabuni hapo alihitaji kufanya kazi na mchezaji huyo kutokana na ubora ambao anajua mchezaji huyo anao na ubora ambao anauleta uwanjani katika michezo ya timu hiyo.

Eric Ten Haag pia ameongeza anavutiwa na namna mchezaji huyo anaboresha kiwango chake kwa siku za hivi karibuni katika kikosi hicho cha mashetani wekundu.

eric ten haagMarcus Rashford ameanza vizuri msimu huu tofauti na msimu uliomalizika kitendo kilichomfanya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tisa wa ligi hiyo na hii inaonesha dhahiri maendeleo ambayo anayaongelea kocha wake.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa