Erik Ten Hag Avunja Ukimya

Kocha wa klabu ya Ajax Erik Ten Hag amevunja ukimya na kukataa kujiondoa kwenye uwezekano wa kutaka kuondoka kwenye ligi kuu ya Uhalanzi kutokana na tetesi zinazoendelea huku akihusihwa na kutaka kuhamia klabu ya Man Utd 

Erik Ten Hag alifanyiwa mahojiano na klabu ya Man Utd wiki iliyopita kulingana na taarifa zilizopo, huku klabu Man Utd ikiaendelea na mchakatao wake wa kutafuta kocha wa kudumu.

Erik Ten Hag

Ten Hag ameifundisha klabu ya Ajax tokea mwaka 2017, kazi yake aliyoifanya kwenye klabu hiyo imewavutia maboss wa United, wanaamini kuwa anaweza kufit kwenye mfumo wa klabu hiyo, ikiwa atapatiwa nafasi ya kuinoa klabu hiyo.

Alipoulizwa kama anaweza thibitisha alifanya mazungumzo na klabu ya man utd alisema, “kila mmoja anajua mwingine kwenye tasnia, kumekuwa na mazungumzo na wawakilishi  kutoka klabu nyingine, hiyo ni kawaida. Manchester United ni klabu kinwa na mashabiki wengi.

“Lakini naweza kurudia mwenyewe, akili yangu iko Ajax. Tayari tumeshapanga kwa ajiri ya msimu ujao.”

Na alipoulizwa tena kuhusu kama amewwka ukomo kuhusu uamauzi wake, alijibu, “nimekaa chini na Ajax kila baada msimu kuisha mpaka sasa. hiyo nayo itafanyika msimu huu.

“Naweza kusema kwamba Ajax na Erik ten Hag wana furaha na kila mmoja kwa kipindi walicho pamoja.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe