Eriksen Awatumia Salamu Wachezaji Denmark.

 

Mchezaji wa Denmark, Christian Eriksen anaendelea kupata ahueni hospitalini na ametuma salamu zake kwa wachezaji wenzake wa timu ya mpira wa miguu ya Denmark.

Eriksen alianguka muda mfupi kabla ya mapumziko katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Euro 2020 ambapo Denmark ilikuwa ikichuana dhidi ya Finland Jumamosi usiku.

Mchezaji huyo wa Inter Milan mwenye umri wa miaka 29 alipata matibabu ya dharura uwanjani kabla ya kupelekwa hospitalini alikolazwa.

 

“Hali yake ni sawa na anaendelea kulazwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi,” ilisema taarifa ya shirikisho la mpira wa miguu la Denmark.

 

“Leo asubuhi tumezungumza na Christian, ambaye ametuma salamu zake kwa wachezaji wenzake.

 

“Timu na wafanyikazi wa timu ya kitaifa wamepokea ushauri nasaha baada ya kushuhudia tukio hilo uwanjani na wataendelea kupeana motisha baada ya tukio la jana.

 

“Tungependa kumshukuru kila mtu kwa salamu zao za dhati.”

Tukio la Jumamosi lilitokea wakati mpira ulipigwa kuelekea kwa Eriksen karibu na mwisho wa kipindi cha kwanza.

Daktari wa timu ya Denmark Martin Boesen alisema Eriksen alikuwa amepoteza fahamu alipomfikia mchezaji huyo uwanjani.

“Nilipomfikia alikuwa amelala upande, alikuwa akipumua, nilihisi mapigo ya moyo, lakini ghafla hilo ilibadilika na tukaanza kumpa CPR,” alisema.

 

“Msaada ulikuja haraka sana kutoka kwa timu ya matibabu na wafanyakazi wengine kwa ushirikiano wao, na tulifanya kile tulichopaswa kufanya na kufanikiwa kumrudisha Christian.”

Mwezi uliopita, Eriksen alisaidia Inter Milan kutwaa taji lao la kwanza la Italia kwa miaka 11 katika msimu wake wa kwanza kamili , baada ya kujiunga na Spurs kwa pauni milioni 16.9 mnamo Januari 2020.

Mchezaji huyo alianza kama mchezaji wa timu ya vijana ya Ajax alihudumu kwa miaka saba akiwa na timu ya ligi ya Uingereza , Tottenham, akiwafunga mabao 69 katika mechi 305 alizoshiriki.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 Komentara

    Safi sana

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

Acha ujumbe