Mshambuliaji wa Borussia Dortmund – Erling Haaland kukaa nje ya uwanja mpaka mwezi Januari baada ya kupata majeruhi ya paja.

Haaland alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Lazio katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kupata majeruhi hayo wakati wa mazoezi.

Kocha wa Dortmund – Lucien Favre anadhani majeruhi ya Haaland yangewezekana kuzuilika endapo kama asingemtumia sana mshambuliaji huyo.

Akizungumza na Sky Germany, Favre amesema “[Haaland] hatocheza mpaka mwanzoni mwa mwezi Januari. Mwanzoni, tulidhani labda sio tatizo kubwa lakini hatoweza kucheza kwa sasa.”

Mpaka sasa, Erling Haaland ameshaitumikia Dortmund katika michezo 14 akianza michezo 13 na amefunga magoli 17 mpaka sasa.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Erling Haaland, Erling Haaland Nje Ya Uwanja Mpaka Januari., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

35 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa