Erling Mchezaji Bora Mwezi

Mchezaji wa klabu ya Manchester City Erling Haaland ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi August baada ya kuwa na mwanzo mzuri huku akiwashinda Pascal Grob wa Brighton, Gabriel Jesus wa Arsenal, Aleksandar Mitrovic wa Fulham, Martin Odegaard wa Arsenal, Nick Pope wa Newcastle, Rodrigo Moreno wa Leeds na Willfred Zaha wa Cystal Palace.

 

Erling Mchezaji Bora Mwezi

Tangu Haaland awasili Uingereza akitokea Borrusia Dortmund, amefunga mabao tisa katika mechi tano za ligi kuu. Hesabu hiyo ndiyo ya juu kabisa kuwahi kusimamiwa na mchezaji katika mechi tano za mwanzo kwenye shindano hili ikijumuisha hattrick mbili mfululizo dhidi ya Crystal Palace na Nottingham Forest.

Raia huyo wa Norway amezidi kuimarika zaidi tangu mwezi ulipoisha, akifunga mabao mawili ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Sevilla kabla ya kucheza na timu yake ya zamani Borrusia Dortmund ambapo alifunga bao lililoipa City alama tatu muhimu.

 

Erling Mchezaji Bora Mwezi

Iwapo Erling atafunga bao kwenye mchezo ujao dhidi ya Wolves unaotarajiwa kupigwa hapo kesho ambapo watakuwa ugenini katika uwanja wa Molineux, Atakuwa mchezaji wa kwanza kupata matokeo katika safari zao nne za kwanza za ugenini kwenye mashindano.

Acha ujumbe