Everton Kumrejea Roberto Martinez?

Baada ya kuachana na Rafa Benitez, Everton ipo kwenye mchakato wa kumpata kocha wa kuiongoza timu hiyo. Roberto Martinez anarudi?

Martinez sio jina geni miongoni mwa mashabiki na wadau wa Everton. Aliwahi kuwa kocha wa klabu hiyo ambapo, alifanikiwa kuifikisha timu hiyo kwenye nafasi ya 5 kabla ya kufululiza kumaliza misimu miwili kwenye nafasi 11.

Nafasi ya 5 ni nafasi kubwa ya mafanikio kwa klabu hiyo kuipata kwenye muongo mmoja uliopita. Safari hii, hali ni mbaya zaidi. Wanaelekea kwenye nafasi zenye hatari ya kushuka daraja, licha ya kufanya usajili mkubwa mwanzoni na katikati mwa msimu huu, yaliyomo hayamo!

Rafael Benitez ameachishwa kazi baada ya kufanya kazi kwa siku 200 pekee.

Ni kama lengo la mashabiki wa Everton kwa Benitez limetimia, hawakumtaka klabuni hapo tangu awali, mara nyingi wamekuwa wakimzomea uwanjani na wakiweka wazi hisia zao za kukasirishwa na maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo kumpatia kazi kocha ambaye  mashabiki hawamtaki, kwao huu ulikua usaliti wa wazi.

Inaripotiwa kuwa, uongozi wa Toffees umeanza hatua za awali za kumtoa Martinez kwenye kibarua chake cha kuiongoza Timu ya Taifa ya Ubelgiji. Swali kubwa ni, Shirikisho la Soka la Ubelgiji litamruhusu Martinez kuachia nafasi yake wakati huu ambao Kombe la Dunia lipo karibuni?

Farhad Moshiri, mmiliki wa Everton.

Wayne Rooney, Frank Lampard na Duncan Ferguson ni miongoni mwa majina yanayohusishwa na kibarua kilichopo kule Goodison Park.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe