Ni uhalisia kuwa, klabu ya Everton inahali mbaya tangu kuondoka kwa Carlo Ancelotti. Sio Rafa Benitez wala Frank Lampard aliyeweza kuirithi mikoba ya Ancelotti, kulikoni?

The Toffees wanahaha kujinasua kwenye kilinge cha kushuka daraja kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 71. Ni tofauti ya pointi 1 tu kati yao na Burnley ambao wapo kwenye nafasi 3 za chini kwenye msimamo wa EPL.

Mvutano mkali kati ya mashabiki na Benitez, uliishia kuona kocha huyo akitimuliwa klabuni hapo na nafasi yake kwenda kwa Frank Lampard. Mashabiki wa Everton walikua wenye furaha na matumaini makubwa na Frankie lakini, ni dhahiri wanachokipitia ni kibaya kuliko enzi za Benitez.

Everton, Everton Mnamvutia Kasi Lampard?, Meridianbet

Ndani ya michezo 8 chini ya Lampard, The Toffees wameshinda michezo 2 na kupoteza michezo 6. Hii ni ishara mbaya kwa uongozi wa klabu hiyo ambao pia, umekua ukinyooshewa vidole na mashabiki wa timu hiyo ambao wameonesha kutokua na imani nao.

Kinachoonekana ni kwamba, bodi ya wakurugenzi wa klabu inamuamini Lampard na, hawaoni kama ni muda sahihi kumuondoa klabuni hapo japokuwa, matokeo na kiwango cha timu kinaonesha kinyume cha haya. Hii ni kusema kuwa, Everton wanamvutia kasi Lampard au wanachokitegemea ni kipi hasa?


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa