Everton Watimua Wanne Tena

Klabu ya Everton wamewafuta kazi makocha wanne wasaidizi ambao walikuwa wanafanya kazi chini ya kocha ambaye wamemfungashia virago Rafa Benitez kwenye dimba la Goodison Park.

Francisco de Miguel Moreno, Antonio Gomez, Jamie Harley na Cristian Fernandez wamefungashiwa virago mara tu baada ya klabu ya Everton kuvunja mkataba na Rafa Benitez kwenye mchezo dhidi ya Norwich City ambapo walipoteza kwa 2-1.

Rafa Benitez ambaye alichaguliwa kuifundisha timu mwezi juni, ameshinnda mchezo mmoja tu kwenye michezo 13 ya ligi kuu ya uingereza, kabla ya kuchaguliwa kuifundisha Everton alikuwa anaifundisha klabu ya Newcastle ambapo nako walimfungashia virago kwa matokeo mabovu.

Everton wanatarajia kuanza mazoezi kesho lakini mpaka sasa hawajamtangaza kocha yeyote ambaye atasimamia mazoezi ya kesho kwenye viunga vya Finch Farm, huku wakijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Aston Villa Jumamosi.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe