Klabu ya Everton imewawekea Man United ngumu kumsajili beki wake kijana Jarrad Branthwaite ambaye Man Uited wamekua wakimuwinda kwa karibu kwajili ya kumsajili kuelekea msimu ujao.
Ofa ya pili ya Manchester United jana ilipigwa chini iliyokua na thamani ya £50 milioni ambapo Everton wameendelea kusisitiza wanahitaji kiasi cha paundi £70 mwisho 65, Jambo ambalo linaweza kuwafanya mashetani wekundu kukimbia dili hilo na kuhamia kwa mchezaji mwingine.Wiki kadhaa nyuma Man United waliripotiwa kupeleka ofa ya paundi milioni 35 kumtaka beki Branthwaite ambayo ilipigwa chini kabla ya jana kutuma ofa ya paundi milioni 50, Ofa hiyo nayo ikapigwa chini kwa muda usiozidi masaa matatu tangu kutumwa kwake.