Beki wa kushoto wa zamani wa klabu ya Manchester United Patrice Evra ametaka kocha wa washambuliaji klabuni hapo Benni Mccarthy apewe sifa anazostahili.
Evra anaamini kazi kubwa ya kuwabadilisha washambuliaji ndani ya klabu ya Manchester United anaifanya Benni Mccarthy, Benni amekua kocha wa washambuliaji wa klabu ya Man United tangu mwazoni mwa msimu akitokea Amazulu ya nchini Afrika ya Kusini.
Kuna mabadiliko makubwa kwa washambuliaji wa klabu ya Manchester United ambao wamekua wakifunga kwa ustadi mkubwa katika michezo tofauti tofauti msimu, Lakini sifa bado haziendi kwa kocha Benni Mccarthy kitu ambacho gwiji Evra anaona sio sahihi.
Marcus Rashford ni miongoni mwa washambuliaji waliokua na mabadiliko makubwa sana msimu huu tofauti na msimu uliomlizika. Msimu huu Rashford ameweza kufunga mabao kwa ustadi mkubwa na hiyo inaonekana ni matokeo ya kocha wa washambuliaji Benni Mccarthy.
Patrice Evra anaamini mabadiliko ambayo mshambuliaji Marcus Rashford anayoonesha ndani ya msimu huu moja kwa moja sifa anastahili kocha Benni Mccarthy, Kwani tangu kuja kwa kocha huyo ndani ya klabu hiyo mwanzoni msimu yameweza kumbadilisha kwa kiwango kikubw mshambuliaji huyo ambaye amehusika kweye mabao 21 mpaka sasa.


