Chama cha soka nchini Uingereza FA kimetangaza sheria mpya ambazo zinakwenda kulinda urithi wa klabu zake zote nchini humo ambapo sheria hizo zitatumika kwenye “premier League, EFL, National League [national division], WomenSuper League na Women Championship.”

Sheria hizo mpya zinatarajiwa kuanza kutimika kuanzia msimu 2022/23, ikifuatia na hatua za ushauri za ligi husika na wadau mbalimbali wa soka nchini humo.

FA, FA Watangaza Sheria Mpya, Meridianbet

Sheria hizo mpya za FA zinazipiga marufuku vilabu vya nchini humo kufanya mabadiliko yoyote kwenye vilabu vyao pasipo kushirikisha wadau wa soka nchini humo, hususani mashabiki.

Ikiwa klabu itakiuka kanuni hizi, basi FA wanahaki ya kuchukua hatua stahiki, kama vile kuaimaru klabu kurudisha mabadiliko ya awali mfano nembo au rangi ya jersey ya nyumbani.

Kusudi la kuanzishwa kwa sheria hii ni kuwaweka mashabiki kuwa sehemu ya maamuzi ya hususani kwenye mambo muhimu ya klabu ambayo yanabeba taswira ya klabu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa