Shirikisho la mpira wa miguu la uingereza FA leo limethibitisha mechi kuendelea kuchezwa kama zilivyopangwa baada ya kuahirishwa wikiendi hii kwa ajiri kido cha Malkia Elizabeth II.
Waraka uliotolewa leo mapema na FA umethibitisha kurudi kwa michezo yote ya soka ndani ya Uingereza wiki hii. Ila kuna wasiwasi wa baadhi ya michezo ambayo itachezwa jijini London kuhairishwa kutokana na shughuri nyingi za mazishi kufanyika jijini humo.
Mpaka sasa kuna wasiwasi wa michezo yote ya itakayopigwa jijini London wiki ijayo kuahirishwa kutokana na mazishi yanayaotarajiwa kufanyika jijini London, ambapo zaidi ya polisi 10000 wanatajiwa kushiriki kwa huduma ya mazishi ya malkia Elizabeth II. Hivyo walinzi wa usalama kwenye viwanja wanaweza wasiwepo au wakapatikana wachache.
Michezo ambayo iko kwenye hatari ya kusimamishwa wikiendi ni Arsenal na Brentfrod, Tottenham na Leicester City, Liverpool na Chelsea, michezo yote hii inatarajiwa kuchezwa jiji London wikiendi hii.
Pia FA imethibitisha kuwa michezo yote ya mpira wa miguu nchini Uingereza ambayo itachezwa siku ya Jumatatu 19, itasimaamishwa kutokana na mazishi ya Malkia Elizabeth II.