Fabian Ruiz amesema kuwa “Asingeweza kukataa” kwa Paris Saint German na anaamini amefanya “chaguo zuri sana” kwa kujiunga na mabingwa hao wa Ligue 1.

 

Fabian Hakuweza Kusema Hapana kwa Psg

Kiungo huyo wa kati wa Uhispania alihamia PSG kwa mkataba wa miaka mitano mwezi uliopita kwa ada ambayo inasemekana iliipa Napoli Pauni Milioni 21.5. Fabian alifichua kuwa ulikuwa uamuzi rahisi kuhamia mji mkuu wa Ufaransa.

Aliiambia El Pais: Ofa inakuja, kati yetu sote tunaamini kuwa ni nzuri sana, kwamba huwezi kusema hapana kwa klabu kama Paris, kwa mradi wanaofanya,  kwa klabu kwa historia.

“Nilikuwa nimebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wangu, na mimi na Napoli tulikuwa na nia ya kuanza mazungumzo, na ninadhani lilikuwa chaguo zuri”

 

Fabian Hakuweza Kusema Hapana kwa Psg

Fabian anafurahia nafasi ya kufanya kazi na wachezaji kama Neymar, Kylian Mbappe na Lionel Messi. Aliongeza kuwa; “Unapofika, inavutia kuona wachezaji bora wakiwa pamoja, kujua kwamba utabadilika nao kwamba utaishi nao kila siku.

“Ni fursa lakini wakati huo huo ni kawaida. Ni watoto wa kawaida”. Fabian ana ushindani mkubwa katika kuingia kwenye kikosi cha Christophe  Galtier,  lakini yupo tayari kutumia nafasi yake Alisema: Wanapenda kile nimekuwa nikifanya miaka hii.

Pale Napoli kwasababu ya kazi au bahati, mambo yalikuwa sawa, kama timu na kibinafsi wananiulza kwa mambo ambayo nimekuwa nikifanya.

 

Fabian Hakuweza Kusema Hapana kwa Psg

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa