Napoli wanaripotiwa kuwa wanajiandaa kumpa ofa ya mkataba mpya Fabian Ruiz kuwazima mabingwa wa La Liga Real Madrid na Barcelona.

Nyota huyu wa Uhispania amevivutia vilabu hivi kutoka nchini kwake na vinara hawa wawili wa La Liga wameripotiwa kupenda kazi yake.

Kwa mujibu wa Calciomercato.com, Rais Aurelio De Laurentiis ameanza kufanyia kazi mkataba mpya kumbakiza staa huyu hadi Juni 2025 kwa kiungo huyo, dili ambalo linatarajiwa kumuongezea mshahara wake wa sasa wa € 1.5m kwa mwaka.

Fabian Ruiz Mkataba Mpya Napoli
Fabian Luiz

Katika mkataba huo mpya, wanatarajia kuingiza kifungu cha kumnunua kwa mkataba wake cha zaidi ya €100m ili kuwakimbiza wanaomfukuzia, wakati nyota huyu wa zamani wa Real Betis akijiendeleza vyema chini ya uongozi wa Gennaro Gattuso pale San Paolo.

Kocha wa zamani wa Betis Quique Setien, ambaye sasa yuko Barcelona, ​​amekuwa akihusishwa na mchezaji huyo lakini Napoli wamedaiwa kuweka dau la € 80m kwa staa huyu mwenye umri wa miaka 24 na hivyo kuwaweka mbali na wanaomvizia.

Mkataba wa sasa wa Fabian huko San Paolo unamalizika mnamo Juni 2023.

36 MAONI

  1. huu ndio muda wa RUIZ kupiga pesa, maana kama zaidi ya vilabu viwili tena vikubwa vinamuhitaji ni ishara kwamba nyota imewaka, akaze buti ataona mafankio

  2. Shida hapo itakuja kwenye ndoto ya mchezaji kuvichezea vilabu hvyo vikubwa viwili na bugana atalolipwa NAPOLI wanaweza shindwa mshawishi kubaki

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa