Fabinho amekiri kuwa ikiwa Liverpool watapata taji la pili, taji hili litakuwa muhimu na la kipekee zaidi ya lile lililopita na litaweka Liverpool kwenye kumbukumbu nzuri ya soka.
Liverpool walitwaa taji lao la kwanza baada ya miaka 30 mwezi Julai, baada ya kuwatupa mbali kwa pointi 18 Man City waliokuwa wakitetea taji hilo.
Msimu huu umekuwa mgumu, na ni mwendelezo wa changamoto zilizoanza tangia msimu uliopita, janga la Corona likiwa ni tatizo kubwa zaidi lililokwamisha sana shughuli za soka.
Msimu huu Liverpool wamekuwa na changamoto ya majeraha, wakimkosa beki wao muhimu Virgil Van Dijk na pia Joe Gomez kwa kipindi fulani.
Lakini Fabinho anaamini kuwa ikiwa watashinda kwa mara nyingine taji la Ligi Kuu ya Uingereza,. basi hili litawapa heshima kubwa zaidi na litakuwa taji la kipekee kwenye historia ya klabu.
” Ukizingatia kila kitu kilichotokea mwaka huu, ugumu wote wa kutokuwa na mashabiki uwanjani na ratiba ngumu za mechi na majeruhi tuliopata, yote haya yanafanya taji la pili kuwa la kipekee zaidi kuliko lile la awali.” – Fabinho
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???
Shakila mrope
Ongera zake
Issa
Si msimu huu
Saupha mohamed
Mambo moto
Adelta
Mambo yanazidi kunoga
Sarah
Mambo yanazidi kuwamoto
Hopemwaikuka
True say
Tatu
Hongera yake
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri sana
Fatuma kasomo
Safi
Mwanahamisi
Hongera zake
Caroline
Kwa kweli litakua si la mchezo
Theonestina
Hongera Sana
Rahmal
Mambo yanazidi kutalaladi
warda
Naombea Man Uwapate jamani
Chiku
Mimi nawapa macho