Fabregas Astaafu Kucheza Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Barcelona na Chelsea Cesc Fabregas ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 36.

 

Fabregas Astaafu Kucheza Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Alisema: “Ni kwa huzuni kubwa kwamba wakati umefika kwangu kutundika viatu vyangu vya kucheza. Kuanzia siku zangu za kwanza Barca, Arsenal, Barca tena, Chelsea, Monaco na Como, nitazithamini zote.”

Fabregas amesema kuwa, Kuanzia kunyanyua Kombe la Dunia, Euro, hadi kushinda kila kitu Uingereza na Uhispania na karibu mataji yote ya Uropa, imekuwa safari ambayo hataisahau.

Fabregas alicheza mechi 739 katika kikosi cha kwanza, akatoa pasi za mabao 217, akafunga mabao 125 na kubeba mataji 17.

Fabregas Astaafu Kucheza Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Msimu huu wa Saba Saba tembelea Duka la Meridianbet lililopo viwanja vya Saba Saba uweze kujua nini ambacho wameleta msimu huu huku kukiwa na nafasi ya kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni kama kupewa bonasi.

Alianza kucheza kwa mara ya kwanza Arsenal akiwa na umri wa miaka 16 na angeendelea kukaa kwa misimu nane katika klabu hiyo, na kubeba Kombe la FA mnamo 2004-05 kabla ya kuhamia Barcelona msimu wa joto wa 2011.

Katika miaka mitatu akiwa na Blaugrana, alishinda taji la LaLiga, Copa del Rey na UEFA Super Cup.

Fabregas Astaafu Kucheza Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Mhispania huyo kisha akarejea Ligi Kuu akiwa na Chelsea, akishinda taji mara mbili, Kombe la FA na Kombe la Ligi kwa The Blues.

Meridianbet mabingwa wa ODDS KUBWA Tanzania wanakwmabia haijaisha mpaka iishe unajiuliza wapi utapiga mkwnaja mrefu?. Basi mahali sahihi ni hapa ingia sasa na uweze kucheza Aviator, Poker, Roulette na mingine mingi.

Pia alicheza mechi 110 kwa Uhispania, akishinda Mashindano ya Uropa mfululizo na Kombe la Dunia.

Fabregas Astaafu Kucheza Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Fabregas sasa atageuka kuwa kocha katika klabu ya Serie B ya Como ambako alicheza mechi 17 msimu uliopita.

Alisema: “Siyo huzuni yote ingawa sasa nitavuka mstari mweupe na kuanza kufundisha timu za B na Primavera za Como 1907. Klabu na mradi ambao sikuweza kuufurahia zaidi.”

Acha ujumbe