Facundo Pellistri Kutolewa United Kwa Mkopo

Mchezaji kinda wa Manchester United, Facundo Pellistri, anaweza kutolewa kwa mkopo klabuni hapo katika dirisha hili la usajili.

Haya yanajiri baada ya wakala wa Facundo Pellistri – Edgardo Lasalvia kuthibitisha Hispania inaweza kuwa ndio sehemu atakayokwenda mchezaji huyo.

Pellistri alisajiliwa na United mwezi Oktoba 2020 akitokea katika klabu ya Penarol inayocheza ligi kuu nchini Uruguay. Licha ya kuwepo kwenye orodha ya wachezaji wa ziada kwenye benchi la United katika mechi 2 za UEFA (PSG na Istanbul Basaksehir), Facundo bado hajacheza mchezo wowote wa EPL.

Facundo Pellistri (kushoto) akishangilia goli lake akiwa na kikosi cha U23 cha Man United.

Mapema wiki hii, mtandao wa Manchester Evening News (MEN), uliripoti utayari wa United kumruhusu Facundo kwenda kucheza kwenye timu nyingine kwa mkopo, lengo likiwa ni kumjengea uzoefu wa kucheza soka la Ulaya.

“Tunalifanyia kazi. Ni kweli, (Facundo) anaweza kwenda Hispania.” Alisema Edgardo baada ya kuulizwa uwezekano wa Pellistri kuondoka United mwezi huu.


USHINDI UPI NI MKUBWA KWAKO, £2,000,000? 🤑

Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.

INGIA MCHEZONI

16 Komentara

    Pole yake

    Jibu

    Usajili umepamba moto

    Jibu

    Pole sana facundo

    Jibu

    Pole san kijana

    Jibu

    Duh hii kali

    Jibu

    Kambi popote facundo kikubwa masrahi tu

    Jibu

    Hii ndio changamoto ya vilabu vikubwa kusajiri wachezaji wengi wasiowahitaji sana mwisho wanaishia kucheza kwa mikopo sehema mbalimbali na anapofanya vzr kwenye club aliyopelekwa na club husika ikataka kumusajiri moja kwa moja tatizo huanzia hapo

    Jibu

    Poleni sana

    Jibu

    Duu pole yake

    Jibu

    Dah

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Sio mbaya akajifunze kwingine huenda pia akapata muda mwingi wa kucheza

    Jibu

    Wampe muda

    Jibu

    Mmmh

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Wamtoe tu sio mbaya

    Jibu

Acha ujumbe