Fadlu Davids Awakataa Wanne

Kocha mpya wa klabu ya Simba Fadlu Davids inaelezwa hajaridhishwa na mwenendo wa wachezaji wanne wa kigeni ndnai ya trimu hiyo kuelekea msimu ujao wa 2024/25.

Fadlu Davids ambaye yupo na kikosi cha Simba kujiandaa na msimu mpya nchini Misri hajaridhishwa na viwango vya wachezaji kama Ayoub Lakred, Fred Michael, Andre Onana, pamoja na Fabrice Ngoma ambapo anahitaji wawekwe nje ya kikosi hicho ikiwezekana na kuletewa wachezaji wengine.fadlu davidsSababu za kutoridhishwa na wachezaji hao ni kuongezeka kwa kilo ambapo hii inatajwa inamhusu golikipa Ayoub Lakred, kutoendana na mahitaji ya mfumo wa timu, Uvivu, lakini pia kukosa nishati ya kutosha kocha huyo anaelezwa anahitaji wachezaji wenye nishati ya hali ya juu kwenye kikosi chake kutokana na aina ya soka lake.

Kutokana na taarifa hizo ni wazi kua kocha Fadlu Davids anahitaji wachezaji ambaoi wanajituma kwa kiwango kikubwa klabuni hapo, Lakini bila kusahau nishati ya hali ya juu kutokana na mfumo wake unavyohitaji na viongozi wa klabu ya Simba kwasasa wanapaswa kurejea sokoni kutafuta wachezaji mbadala wa hao waliotajwa kutomridhisha kocha kabla ya dirisha kufungwa.

Acha ujumbe