Wababe wa Ulaya wanaendelea kujipanga kwaajili ya kukamilisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambayo ni michuano inayoheshimika ulimwenguni, hivi ni baadhi ya vitu unavyopaswa kuvifahamu.
Fainali ya UEFA: Wapi, Lini na Idadi ya Wahudhuriaji
Timo Werner (kushoto) na Raheem Sterling (kulia)

Lini Fainali ya Ligi ya Mabingwa itachezwa?

Fainali ya Champions League ambayo itazikutanisha timu mbili kutoka Uingereza (Chelsea dhidi ya Manchester City) itachezwa siku ya Jumamosi tarehe 29 Mei 2021.

Wapi Fainali ya Ligi ya Mabingwa Itachezwa?

Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2021 itapigwa katika dimba la Estadio do Dragao huko Porto, nchini Ureno. Uwanja wa nyumbani wa Porto wanaocheza ligi ya Premeira Liga na unawezo wa kubeba mashabiki 50,000.

Fainali ya UEFA: Wapi, Lini na Idadi ya Wahudhuriaji

Mwanzo ilikuwa fainali hii ichezwe nchini Uturuki, Instanbul katika uwanja wa The Ataturk Olympic Stadium lakini UEFA imeamua kuhamishia Portugal kufuatia maamuzi ya serikali ya UK sababu ya sheria za kujikinga na Covid-19.

Inakuwa ni mara ya pili mfululizo fainali za michuano hiyo kuchezwa nchini Ureno baada ya fainali iliyopita kuchezwa katika uwanja wa Estadio da Luz huko Lisbon.

“Mashabiki wamelazimika kuteseka zaidi ya miezi kumi na mbili bila kuzishuhudia timu zao na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa ni kilele cha mpira wa miguu klabuni,” alisema rais wa UEFA Aleksander Ceferin.

Idadi ya Mashabiki Watakaoruhusiwa Kuhudhuria Fainali ya UCL 2021:

Mashabiki wataruhusiwa kuhudhuria fainali ya Ligi ya Mabingwa kufuatia uamuzi wa UEFA kuhamishia mchezo Ureno.

Wakati uwezo wa mwisho bado haujathibitishwa, UEFA inasema kuwa vilabu vitapokea mgao wa tiketi 6,000 kila moja (Jumla 12,000), na umma kwa ujumla watakua huru kununua tiketi kutoka Mei 24.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Fainali, Fainali ya UEFA: Wapi, Lini na Idadi ya Wahudhuriaji, Meridianbet

CHEZA HAPA

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa