Fainali za Kombe la EFL 2020/21 Zimesogezwa Mbele

Fainali za kombe la EFL 2020/21 zimesogezwa mbele kutoka mwezi Februari kwenda Aprili ili wanaweza kuhusisha mashabiki wengi iwezekanavyo.

Fainali hizi awali zilitarajiwa kuwa zingefanyika Februari 28, 2021, lakini kumekuwa na changamoto zaidi kutokana na janga la Corona.

Janga hili limeendelea kuwa changamoto kwa ushiriki wa mashabiki kwenye viwanja vya soka nchini Uingereza, wakati EPL wakiwa wameshaanza kuruhusu idadi ndogo ya mashabiki.

Kwa mujibu wa EFL, wanaamini hadi kufikia mwezi Aprili kutakuwa na mabadiliko ambayo yanaweza kuwaruhusu mashabiki kusafiri na kuhudhuria viwanjani.

“Idadi ya mashabiki watakaoruhusiwa inategemea muongozo unaowekwa na serikali, tunaamini kusogeza tarehe mbele mwakani kutatoa fursa nzuri kwa timu na mashabiki kuhudhuria.” -Taarifa ya EFL

Kwa sasa michuano ya EFL ipo katika hatua ya robo fainali. Huku mabingwa watetezi Manchester City wakitarajia kuumana na Arsenal Jumanne hii, wakati Brentford wakiwakaribisha Newcastle United. Tottenham naye dhidi ya Stoke City, pia Manchester United wakisafiri kumenyana na Everton Jumatano.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

18 Komentara

    Corona inaharibu

    Jibu

    Corona imeharibu sana

    Jibu

    Hili janga la corona limeharibu mambo mengi san

    Jibu

    Duuu huu ugonjwa ni shidaa

    Jibu

    Corona imeharibu Mambo mengi sana

    Jibu

    Corona imevuruga mambo

    Jibu

    Corona imeharibu sana tasnia ya michezo mashabiki wamekosa burudani live

    Jibu

    Bora hvyo

    Jibu

    Corona noma

    Jibu

    Coronavirus imeharibu mambo mengi
    Kubwa zaidi kwenye ulimwengu wa soka

    Jibu

    Covid 19 ni tishio

    Jibu

    Corona cyo poa

    Jibu

    Duu sio poa

    Jibu

    Kwa mujibu wa EFL, wanaamini hadi kufikia mwezi Aprili kutakuwa na mabadiliko ambayo yanaweza kuwaruhusu mashabiki kusafiri na kuhudhuria viwanjani.

    Jibu

    Duuh

    Jibu

    Duh nouma Sana

    Jibu

    Corona sio poa

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

Acha ujumbe